Watu wanaodaiwa kuwa ni majangili na wawindaji haramu
wameitungua kwa risasi helkopta ya doria ya wanyamapori katika pori la
akiba la maswa lililoko wilaya ya Meatu mkoani Simiyu kusini mwa hifadhi
ya taifa ya Serengeti na kumuua rubani wa helkopita na kumjeruhi askari
mmoja wa wanayamapori.
Kufuatia tukio hilo, waziri wa maliasili na utalii Profesa
Jumanne Maghembe amefika katika eneo la tukio na kusisitiza kwamba
serikali kwa kushirikiana na vyombo vyote vya dola na vyombo vya ulinzi
na usalama inaanzisha mkakati mpya wa kupambana na ujangili na uwindaji
haramu wa maliasili ikiwemo Tembo ambao ni rasilimali muhimu kwa taifa
na kwa uhifadhi wa taifa la Tanzania.
Waziri Maghembe ambae amefika kwenye eneo hilo
ilipotunguliwa helkopita hiyo katika safari iliyokuwa na msukosuko mingi
ya barabara na hasa kipindi hiki cha mvua na kuikuta helkopita
iliyokuwa inarushwa na kepten Roger Gower raia wa Uingereza ambae
alifariki baada ya kujeruhiwa kwa risasi amesema tukio hilo limewakera
wadau wote wa uhifadhi na serikali kwa ujumla na kamwe haliwezi kuachwa
lipite bila hatua madhubuti kuchukuliwa huku akiwaonya baadhi ya
watumishi wa serikali na askari wa wanyamapori wanaoshirikiana na
wahalifu kuwa sasa kiama chao kimefika.
Nae kamanda wa upelelezi wa mkoa wa Simiyu Jonathan Shana
amesema tukio hilo lilitokea jana jioni wakati helkopita hiyo ikiwa
katika doria baada ya kusikika milio ya risasi ya majangili katika pori
hilo ambapo Tembo watatu waliuwawa na kwamba watu watatu wanashikiliwa
na polisi wakihojiwa kufuatia tukio hilo ambapo mkurugenzi mkuu shirika
la hifadhi za taifa Tanzania Tanapa Allan Kijazi amesisistiza umuhimu wa
wadau kuongeza nguvu katika kukabiliana na matatizo ya ujangili nchini.
Hakuna maoni :