SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / Hii ndio Idadi ya Kura Alizopata Samata – Na Namna Kura Zilivyopigwa


Mbwana Samatta ndio jina liliotajwa zaidi kwenye vinywa vya watanzania wengi na Afrika kiujumla ndani ya masaa kadhaa yaliyopita – baada ya mwanasoka huyo wa Kitanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika Anayecheza Ligi za Ndani ya Afrika.

  Ushindi wa Samatta, ambaye ni mshindi wa na mfungaji bora wa ligi ya mabingwa wa Afrika umetokana na kuwashinda wapinzani wake Zein Edin Farahat, Roger Assale, Robert Kidiaba, Moudather el Tahir,Mohammed Meftah, Kermit Erasmus, Felipe Ovono, Baghdad Bournedjah, na Abdeladim Khadrouf.

Utaratibu wa CAF – Shirikisho la soka katika upigaji kura wa kumchagua mshindi wa tuzo hii unatokana na kura zilizopigwa na makocha wa timu za taifa au wakurugenzi wa ufundi wa vyama vya soka vya nchi za kiafrika.

Kwa mwaka huu wachezaji wote hao waliotajwa hapo juu walipigiwa kura na matokeo ni kama yanavyoonekana kwenye mpangilio hapo chini.

Mbwana Samatta alipata jumla ya kura 127 na hivyo kuongoza, akifuatiwa kwa mbali na mchezaji mwenzie wa TP Mazembe Robert Kidiaba aliyepata kura 88 na aliyefunga Top 3 ni  Baghdad Bournedjah. Kura zilipigwa na mataifa 45 ya nchi wanachama wa shirikisho la soka Afrika CAF.

Kwa upande wa Tuzo aliyoshinda Aubemayang kura zilikuwa hivi:

 1- @Aubameyang7 143 points

2- @YayaToure 136 points

3- @AyewAndre 112 points



Mbwana Samatta pia alifanikiwa kutajwa katika kikosi bora cha Afrika cha mwaka 2015

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply