Tumeshuhudia watuhumiwa wa Escrow wakikabidhiwa Wizara na Idara Muhimu
za Umma na wengine kupitishwa kugombea Ubunge wa kwenye Serikali ya
awamu wa Tano kana kwamba hawakufanya Ufisadi wa aina yoyote, kwenye
Serikali ya awamu wa nne. Pengine mimi naweza kuwa sina Ufahamu wa
kutosha juu ya maana ya neno Ufisadi.
Hebu tujiulize, unawezaje kufumbia macho Ufisadi wa Escrow zaidi ya
bilioni 300, na wakati huo huo ukasema unatumbua jipu kwa ufisadi
bilioni 59? Namaanisha bilioni 12 za makontena TRA na 47 za makontena
bandarini. Na usimpeleke mtu hata mmoja mahakamani, na wakati huo huo
ukamkabidhi uongozi, Wizara na Idara muhimu za Umma.
Kwa uelewa wangu hapa kuna double standard na maana halisi ya Kutumbua jipu inageuka kuwa uonevu na kuoneana haya.
Je, ni lini watuhumiwa hawa wa Escrow walifikishwa mahakamani kujibu
tuhuma za Ufisadi wa Escrow na Mahakama ikawasafisha, na wakastahili
Promotion hii?
Prof. Muhongo - Waziri Nishati na Madini
Maswi - Ag D. Commissioner TRA.
Chenge - Mbunge.
Tibaijuka - Mbunge.
Ngeleja - Mbunge.
Je, Escrow ni Ufisadi au Promotion?
" Injustice anywhere is a threat to justice everywhere" M.L. King Junior.
Tagged with: MATUKIO
Hakuna maoni :