Kocha Jose Mourinho ameibukia nchini China katika jiji la Shanghai ambako haijajulikana alichokifuata.
Lakini
kocha huyo wa zamani wa Chelsea, amekumbana na shabiki ambaye
amemkumbisha machungu baada ya kumkabidhi jezi ya Chelsea ili asaini.
Shabiki
huyo wa kike wa soka, alimfuata Mourinho akiwa na jezi ya Chelsea na
kumpa mkononi ili asaini. Mourinho raia wa Ureno, hakuwa na kinyongo,
akaichukua, akasaini na kumrejeshea.
Chelsea ilimtupia Mourinho virago baada ya kikosi chake kuboronga kinoma, msimu mmoja tu baada ya kutwaa ubingwa.





Hakuna maoni :