SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / KEPTENI ROONEY AIZAMISHA LIVERPOOL ANFIELD, AWEKA REKODI ENGLAND.

LIGI KUU ENGLAND
Ratiba/Matokeo:
Jumapili Januari 17
Liverpool 0 Man United 1         
  

MANUNITED-ROONEY-GOLI-LIVERBAO la Kepteni Wayne Rooney, la kwanza kabisa Uwanjani Anfield tangu 2005, Leo limewapa Manchester United ushindi wa 1-0 dhidi ya Mahasimu wao Liverpool katika Mechi ya Ligi Kuu England.

Liverpool walitengeneza nafasi nyingi katika Mechi hii lakini Kipa David De Gea na umaliziaji BPL-JAN17Awao mbovu ndio vilikuwa vikwazo na Man United kufunga Bao lao la ushindi katika Dakika ya 78 kwa Shuti lao pekee katika Mechi nzima lililolenga Golini.

Goli hilo lilitokana na Kona ambapo Marouane Fellaini alipiga Kichwa kilichogonga Posti na Mpira kuwahiwa na Wayne Rooney na kutinga.

Hilo ni Bao lake la 5 katika Mechi 4 zilizopita na ni la 176 kwenye Ligi Kuu England ambalo limemfanya sasa awe anashikilia Rekodi ya kuwa Mfungaji wa Bao nyingi kwenye Ligi Kuu England akichezea Klabu 1 tu akifuatiwa na Thierry Henry mwenye 175 alizofunga akiiichezea Arsenal pekee.

Matokeo haya yameipandisha Man United Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 2 tu nyuma ya Timu ya 4 Tottenham wakati Liverpool wapo Nafasi ya 9 Pointi 8 nyuma ya Tottenham.

VIKOSI:
Liverpool: Mignolet; Clyne, Toure (Benteke - 81'), Sakho, Moreno; Lucas, Henderson, Can; Milner (Caulker - 90'), Lallana (Ibe - 76'); Firmino
Akiba: Ward, Caulker, Smith, Allen, Teixeira, Ibe, Benteke.

Manchester United: De Gea; Young (Borthwick-Jackson - 42'), Smalling, Blind, Darmian, Schneiderlin, Fellaini; Lingard (Mata - 66'), Herrera (Depay - 72'), Martial; Rooney
Akiba: Romero, Borthwick-Jackson, McNair, Varela, Pereira, Mata, Depay.

REFA: Mark Clattenburg
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
**Saa za Bongo            
Jumatatu Januari 18
2300 Swansea v Watford   

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply