SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / NYOTA AFRIKA: SHUJAA WA TANZANIA SAMATTA NA AUBAMEYANG, NDIO BORA AFRIKA.


SAMATTA-AUBAMEYANGKwa mara ya kwanza Afrika imechagua Wachezaji wapya kabisa kuwa ndio Nyota Bora wa Mwaka baada ya Mastraika wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang, na wa Tanzania, Mbwana Samatta, kuzoa Tuzo hizo.

Samatta, Supastraika Mtanzania anaechezea Klabu ya TP Mazembe ya Congo DR ambayo aliifanikisha kutwaa Ubingwa wa Afrika huku yeye akiibuka Mfungaji Bora, alishinda Tuzo hiyo kwa Wachezaji wachezao ndani ya Afrika kwa kuzoa Pointi 127 akiwaangusha Mchezaji mwenzake wa TP Mazembe Kipa Robert Muteba Kidiaba, aliepata 88 na Mchezaji wa Algeria, Baghdad Bounedjah alieambua 63.

Kwa upande wa Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa wachezao Soka nje ya Afrika, Mchezaji wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang, anaechezea Borussia Dortmund, alimbwaga Yaya Toure wa Ivory Coast na Man City baada kuzoa Pointi 143 zikiwa 7 zaidi ya Toure ambae alitwaa Tuzo hii mara 4 mfululizo.

Andre Ayew wa Ghana alipata 112 na kumaliza nafasi ya 3.
Samatta na Pierre-Emerick Aubameyang wanakuwa Wachezaji wa kwanza kabisa kwa Nchi zao kutwaa Tuzo hizi.

***ZA AWALI:
SHUJAA WA TANZANIA-MBWANA SAMATTA, NDIE BORA AFRIKA!
Mbwana Ally Samatta Usiku huu huko Abuja, Nigeria ametunukiwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Mwaka 2015 kwa wale wachezao ndani ya Afrika na kuandika Historia Tanzania.

HII NI FURAHA KUBWA NA KITU CHA KUJIVUNIA KWA NCHI YETU!
selasinihabari TUNAMPA PONGEZI NA DUA ZETU ZOTE, SIKU ZOTE ZIKO KWAKE!
MOLA AKUBARIKI!
MOLA AIBARIKI TANZANIA!
Aminia!
***HABARI ZAIDI TUTAWAJUZA BAADAE

HABARI ZA AWALI:
ALHAMISI JAN 7 ABUJA: SAMATTA KUZOA TUZO MCHEZAJI BORA AFRIKA?
STRAIKA MAHIRI wa Tanzania Mbwana Ally Samatta yupo huko Abuja, Nigeria kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Mwaka kwa wale wachezao ndani ya Afrika ambapo Mshindi wake atatangazwa Alhamisi Januari 7.

Samatta, anaechezea Klabu Bingwa ya Afrika TP Mazembe ya Congo DR, alifunga Bao 7 kwa Mazembe zikiwemo Bao 2 wakati wa Fainali ya kutwaa Ubingwa wa Afrika.

Wachezaji wengine Wawili watakauchuana na Samatta kuwania Tuzo hii ni Mchezaji mwenzake wa TP Mazembe, Kipa Robert Kidiaba na Mchezaji kutoka Algeria anaechezea Etoile Du Sahel, Baghdad Boundjah.

3 Bora ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Mwaka wale Maprofeshenali wa nje itagombewa na Andre Ayew (Ghana/Swansea City), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon/Borussia Dortmund) na Yaya Toure (Cote d"Ivoire/Manchester City)
Washindi wa Tuzo hizi, ambao hupatikana kwa Kura za Makocha Wakuu au Wakuu wa Ufundi wa Vyama Wanachama wa CAF, watatangazwa Leo kwenye Hafla maalum iitwayo Glo-CAF Awards Gala huko Abuja, Nigeria.

Mchezaji Bora Afrika wa Mwaka
Andre Ayew (Ghana/Swansea)
Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon/ Borussia Dortmund)
Yaya Toure (Cote d"Ivoire/ Manchester City).

Mchezaji Bora Afrika wa Mwaka – wanaocheza ndani ya Afrika
Baghdad Boundjah (Algeria/: Etoile du Sahel)
Mbwana Ally Samata (Tanzania/ TP Mazembe)
Robert Kidiaba (DR Congo/ TP Mazembe)

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply