SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / REAL, ATLETICO KUIKATIA RUFAA ADHABU YA FIFA KUTOSAJILI WACHEZAJI WAPYA.

REAL-ATLETI2VIGOGO wa Jiji la Madrid ambao ni Mahasimu wakubwa, Real Madrid na Atletico Madrid, zimetangaza kukata Rufaa kupinga Adhabu ya FIFA ya kuzipiga marufuku kusaini Wachezaji wapya kwa vipindi viwili vijavyo vya Madirisha ya Uhamisho ukiondoa hiki cha sasa ambacho wanaruhusiwa.


Klabu zote mbili zimeadhibiwa kutokana na kukiuka Sheria za Uhamisho wa Kimataifa na Usajili wa Wachezaji wa chini ya Miaka 18.

Mara baada ya kutangazwa Adhabu hiyo ya FIFA, Real walitoa Taarifa ndefu kwenye Tovuti yao na kupinga Adhabu hiyo waliyodai ni uonevu na kutoa azma yao ya kukata Rufaa FIFA na ikibidi CAS [Court of Arbitration for Sport], Mahakama ya Usuluhishi Michezoni.

Kwa mujibu wa Real, wao walisajili Wachezaji wote wa chini ya Miaka 18 kisahihi kabisa na wakasajiliwa kwa RFEF, Shirikisho la Soka la Spain, ambalo nalo liliwasilisha Usajili huo kwa FIFA.

ADHABU YENYEWE:
-Kutosajili Wachezaji kwa Mwaka mmoja [Madirisha ya Uhamisho ya Julai-Agosti 2016 na Januari 2017
-Faini: Atletico Pauni 620,000 na Real Pauni 250,000.

-HAIKATAZWI:
-Kusaini na Kusajili Wapya Dirisha la Uhamisho la sasa linaloisha Februari 1.
-Klabu hizi zinaweza kusaini Wachezaji wapya wakati wowote wa Adhabu yao lakini Wachezaji hao hawatasajiliwa na hivyo hawataruhusiwa kucheza hadi baada ya Juni 2017.
-Klabu hizi ruksa kuuza Wachezaji wao wakati wowote ule.


Nao Atletico Madrid pia wametangaza kukata Rufaa ingawa Rais wa Klabu hiyo, Enrique Cerezo, amesisitiza Adhabu ya kutosajili Wachezaji wapya haitawaathiri.

Real na Atletico zimefuata mkumbo wa Barcelona waliopewa Adhabu za aina hiyo kutoka FIFA walipofungiwa kusaini Wachezaji wapya kwa Mwaka mzima Mwezi Aprili 2014 kwa kosa hilo hilo la kukiuka Sheria za Uhamisho wa Kimataifa na Usajili wa Wachezaji wa chini ya Miaka 18.

Kufuatia Adhabu hiyo, Barcelona walikata Rufaa kwa FIFA na baadae kwa CAS [Court of Arbitration for Sport], Mahakama ya Usuluhishi Michezoni, lakini Rufaa zao zote zikatupiliwa mbali na wakatumikia Adhabu yao ambayo imeisha Januari hii.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply