Straika
nyota nchini Mbwana Samatta anayekipiga katika kikosi cha TP Mazembe,
ameteuliwa kuwa nahodha moywa wa kikosi cha Taifa Stars.
Uteuzi
huo unahitimisha zaidi ya miaka mitano ya unahodha wa Stars kwa Nadir
Haroub ‘Cannavaro’ ambaye ni nahodha wa Yanga pia Zanzibar Heroes.
Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa, amesema Samatta ndiye nahodha mpya wa kikosi chake.
“Samatta ndiye nahodha mpya wa Taifa Stars, haya ni mabadiliko ya kawaida kabisa,” alisema Mkwasa.
Mara
ya mwisho, Cannavaro aliiongoza Stars akiwa nahodha baada ya kufungwa
mabao 7-0 dhidi ya Algeria katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la
Dunia.
Hakuna maoni :