SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / VPL: YANGA YALIZWA TANGA NA COASTAL, SIMBA DAR KIDEDEA NA SPORTS, MVUA YAIVUNJA MECHI YA MTIBWA NA STAND UNITED.

LIGI KUU VODACOM
Ratiba/Matokeo:
Jumamosi Januari 30
Coastal Union 2 Yanga 0
Simba 4 African Sports 0
JKT Ruvu 0 Majimaji 0
Tanzania Prisons v Azam FC [IMEAHIRISHWA]
Mtibwa Sugar 1 Stand United 0 [Mechi imeahirishwa kutokana na Mvua]
Mwadui FC 1 Toto Africans 0
Kagera Sugar v Mbeya City

VPL-SIT-LOGOMabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Vodacom, VPL, Yanga Leo huko Mkwakwani Jijini Tanga wamecharazwa Bao 2-0 na Coastal Union na simanzi imezidi kwao baada ya Watani zao Simba kuicharaza African Sports Bao 4-0 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Bao za Simba hii Leo zilifungwa na Hamisi Kiiza, Bao 2, Messy na Ugando.
Huko  Tanga, Bao za Coastal Union ziliingizwa na Miraj Adam na Juma Mahadhi katika kila Kipindi kwenye Mechi ambayo Yanga walimaliza Mtu 10 baada ya Beki wao Kevin Yondani kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
 
Hiki ni kipigo cha kwanza kwa Yanga kwenye VPL Msimu huu lakini wamebaki wakiongoza Ligi hiyo wakiwa Pointi sawa na Azam FC ambao sasa wamecheza Mechi 1 pungufu ya Yanga.

Simba wao wanabaki Nafasi ya 3 lakini pengo lao na Timu ya Pili Azam FC na Vinara Yanga sasa ni Pointi 3 tu.
Huko Manungu, Morogoro, Mechi kati ya Mtibwa Sugar na Stand United ilivunjika kutokana na Mvua kubwa huku Mtibwa Sugar wakiwa mbele kwa Bao 1-0.
Mechi hii sasa itamaliziwa Kesho kwa Dakika zilizobaki.
LIGI KUU VODACOM
Ratiba:
Jumapili Januari 31
Mgambo JKT v Ndanda FC
Jumatano Februari 3
Kagera Sugar v Majimaji
Tanzania Prisons v Yanga
Simba v Mgambo JKT
JKT Ruvu v Mbeya City
African Sports v Mwadui FC
Mtibwa Sugar v Toto Africans
Azam FC v Stand United
Coastal Union v Ndanda FC
Jumamosi Februari 6
Kagera Sugar v Simba
Mbeya City v Tanzania Prisons
JKT Ruvu v Yanga
African Sports v Stand United

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply