SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / YAANGA YAANZA KUTOA FUNZO KWA MAFUNZO KOMBE LA MAPINDUZI, NGOMA ANG'ARA


Yanga imeanza michuano ya Mapinduzi kwa kishindo kwa kuitwanga Mafunzo kwa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, leo.

Mabao mawili ya Yanga yamefungwa na Donaldo Ngoma aliyepewa pasi na Mzimbabwe mwenzake Thabani Kamusoko katika dakika za 31 na 34 na kuifanya Yanga kwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili, Mafunzo walijitutumua na kupeleka mashambulizi kadhaa likiwemo lililozaa penalti baada ya Kelvin Yondani kuachwa na kumvuta mshambuliaji wa Mafunzo, lakini kipa Deo Munishi ‘Dida’ akaipangua na baadaye kuidaka.

Paul Nonga aliyeingia dakika 10 za mwisho kuchukua nafasi ya Tambwe alifunga bao la tatu katika dakika ya 90 huku walinzi wa Mafunzo wakiamini alikuwa ameotea.


Mechi nyingine baadaye ni kati ya Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo inatarajiwa kuwa mechi ngumu na ya kusisimua zaidi kutokana na upinzani mkali wa timu hizo katika Ligi Kuu Bara.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply