Baada
ya kutoka Sare 0-0 hapo Januari 30 huko Anfield, Jijini Liverpool, West
Ham na Liverpool sasa zitarudiana Jijini London Uwanjani Upton Park
katika Mechi ya Raundi ya 4 ya EMIRATES FA CUP.Mshindi wa Mechi hii atasonga Raundi ya 5 na kucheza Ugenini hapo Februari 21 na Blackburn Rovers.
Mechi nyingine ya Marudiano ya Raundi ya 4 ya Kombe hili itachezwa Jumatano kati ya Peterborough na West Brom na Mshindi wake kucheza Raundi ya 5 Ugenini na Reading.
Uso kwa Uso – Mechi 3 zilizopita:
FA Cup, Januari 2016
Liverpool 0 West Ham 0
Ligi Kuu England, Januari 2016
West Ham 2 (Carroll, Antonio) Liverpool 0
Ligi Kuu England, Agosti 2015
West Ham 3 (Lanzini, Noble, Sakho) Liverpool 0
Mechi za Raundi ya 5 ya EMIRATES FA CUP zitachezwa kuanzia Jumamosi Februari 20 na kumalizika Jumatatu Februari 22.
EMIRATES FA CUP
Ratiba
Raundi ya 4 Marudiano
Jumanne Februari 9
2245 West Ham v Liverpool
Jumatano Februari 10
2245 Peterborough v West Brom
Raundi ya 5
Jumamosi Februari 20
1545 Arsenal v Hull
1800 Reading v West Brom au Peterborough
1800 Watford v Leeds
2015 Bournemouth v Everton
Jumapili Februari 21
1700 Blackburn v Liverpool au West Ham
1800 Tottenham v Crystal Palace
1900 Chelsea v Man City
Jumatatu Februari 22
Shrewsbury v Man United
THE EMIRATES FA CUP 2015/16
TAREHE MUHIMU
Raundi ya 5
Jumamosi 20 Februari 2016
Raundi ya 6-Robo Fainali
Jumamosi 12 Machi 2016
Nusu Fainali
Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016
Fainali
Jumamosi 21 Mei 2016

Hakuna maoni :