| MANJI |
Kikosi cha Yanga sasa kinaondoka Ijumaa kwenda nchini Mauritius kwa ajili ya mechi yake ya Ligi ya Mabingwa.
Awali, uongozi wa Yanga, jana uliwatangazia waandishi wa habari kwamba Yanga itaondoka leo alfajiri.
Taarifa
zinaeleza kwamba, Manji ameamua kuikodia Yanga ndenge maalum baada ya
kupata taariafa kungekuwa na suala la wachezaji wa Yanga kukaa uwanja wa
ndege kwa saa saba na pia wakati wa kurudi wangelezimika kulala
Johannesburg.
Lakini
Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amesema kwamba kamati ya mashindano
imeshauriana na uongozi na kuona ni muhimu timu ikiondoka Ijumaa.
“Nisingependa
kuzungumzia suala la nani kakodi ndege, wewe jua Yanga sasa itaondoka
Ijumaa badala ya leo kwa sababu hizo za kiufundi.
“Uongozi
na kamati ya ufundi imeona ni bora wachezaji waondoke Ijumaa kwa ajili
ya kupunguza uchovu. Kama wangeondoka leo, saa saba pale uwanja wa ndege
lisingekuwa jambo zuri kwa afya ya mchezaji.
“Angalia,
wangeondoka alfajiri, wangefika Afrika Kusini saa mbili na nusu hivi.
Halafu wangeendelea kuwa uwanja wa ndege hadi saa nane mchana kusubiri
ndege ya kwenda Mauritius.
“Hivyo
Ijumaa ndiyo siku sahihi, tutatumia saa nne tu hadi Mauritius na baada
ya hapo ndege itakuwa ikitusubiri na tutageuza nayo,” alisema Muro.

Hakuna maoni :