| SIMBA |
N
Gumzo kubwa katika vitongoji vya mji wa Shinyanga ni kuhusiana na mechi ya Simba dhidi ya wenyeji wake Stand United.
Mechi hiyo itachezwa Jumamosi na tayari Simba wako mjini hapa huku vijiwe vingi gumzo likiwa ni mechi hiyo.
Simba ilicheza mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Kambarage mjini hapa na kuitwanga Kagera Sugar kwa bao 1-0.
Sasa
ni zamu ya wenyeji ambao wanataka kujiweka sawa na kumuonyesha kazi
mnyama Simba ambaye anaonekana kuamka na kushinda mechi tano mfululizo
za Ligi Kuu Bara.
Lakini Stand wamekuwa wakijitapa, watakuwa wa kwanza kuisimamisha Simba ya kocha Jackson Mayanja raia wa Uganda.
Lakini Mayanja, amesema kikosi chake kinachotaka ni ushindi ili kuendeleza rekodi nzuri.
“Ushindi
litakuwa jambo zuri, tunaamini kupumzika kutatusaidia tofauti na
ilivyokuwa mechi dhidi ya Kagera, wachezaji walichoka baada ya kucheza
mechi mfululizo,” alisema Mayanja.
| STAND |
Lakini Kocha Mfaransa, Patrick Liewig anaamini pamoja na ubora wa Simba, Stand United itawashangaza.
“Timu
yangu in a vijana wengi zaidi. Tumefanya maandalizi mazuri, licha ya
kuwa na majeruhi kadhaa, lakini tutawashangaza,” alisema.

Hakuna maoni :