Kwa
masikitiko makubwa tukio tajwa hapo chini limetokea Chuo cha SAUT
Mwanza ambapo Jamaa wa jinsia ya kiume ,alienda kumtembelea mpenzi wake
chuoni SAUT bweni la RUGAMBWA,
Ukweli
ni kwamba huyo jamaa na huyo demu ni wapenzi wa muda mrefu na pia jamaa
sio mwanafunzi ni raia wa kawaida anayehusika na mambo hasa ya modeling
na amekuwa akiandaa event mbalimbali kama mtakuwa na kumbukumbu vizuri
kuna kipindi kulitokeaga shindano la MISS ALBINISM lililofanyika Mwanza
huyu jamaa alikuwa miongoni mwa wahusika wa hilo shindano,na siku tatu
zilizopita huyu jamaa alitoka kumzika baba yake mzazi.
Kilichotokea
hapo ni baada ya jamaa kwenda hosteli za wanawake ambazo zipo ndani ya
chuo ambapo ndipo alipokuwa akiishi huyo demu wake, katika kukagua simu
ndipo akakuta sms za utata, ukatokea ugomvi katika mabishano demu
akasema atamwita mwizi kama utani kweli demu akaita mwizi.
Jamaa
kwa kuogopa na sababu hakuwa na kitambulisho ndipo akatoka mbio, hapo
ndipo alipoharibu wananzengo na wanachuo bila kujali wakaanza kupiga na
mpaka wanafika polisi alikuwa kapigwa sana, alipelekwa kituoni kutoa
maelezo. Baada ya hapo ndipo tukapata taarifa kafariki na hiyo ni sababu
ya kipigo.
Hakuna maoni :