Mtoto wa Afghanistan aliepata umaarufu Duniani baada ya kupigwa Picha akivaa Jezi iliyotengenezwa kienyeji kwa Mfuko wa Plastiki wa Rangi za Argentina na Jina la Messi huku pia ikiwa na Namba 10 sasa amekabidhiwa Jezi halisi na Lionel Messi mwenyewe ambayo ameisaini.
Mtoto
huyo mwenye Miaka Mitano aitwae Murtaza Ahmadi anampenda mno Messi
lakini Familia yake ya Kimaskini inayoishi Jimbo la Ghazni Jirani na Mji
Mkuu wa Afghanistan, Kabul, Nchi ambayo ina misukosuko ya vita, haina
uwezo wa kununua Jezi Orijino ya Staa huyo wa Argentina.
Kaka
wa Murtaza, Homayoun, mwenye Miaka 15, aliamua kumtengenezea Mdogo wake
Jezi ya Argentina kutoka Mfuko wa Plastiki na kuiandika Jina la Messi
na Namba 10 kwa Peni na kisha kuiposti Picha yake kwenye Mtandao wa
Facebook Mwezi uliopita.
Picha hiyo ilizagaa mno Dunia nzima na kuwa maarufu kupindukia.
Wiki
kadhaa zilizopita, Jorge Messi, Baba Mzazi wa Lionel Messi, alisema
Lionel Messi anajua kuhusu Picha hizo na anataka kufanya kitu kwa ajili
ya Shabiki wake huyo Mtoto wa Afghanistan ikiwa pamoja na kukutana nae.
Mtoto huyo mbali ya kupewa Jezi halisi, pia amepewa Mpira.
Habari
hizi zimethibitishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto Tawi la
Afghanistan, UNICEF, ambalo liliposti Twitter iliyosema: “Murtaza ana
kitu halisi. Leo Messi amesaidia kuifanya ndoto yake iwe kweli na
kumkabidhi Jezi iliyosainiwa na Mpira.”
Hakuna maoni :