| CANNAVARO |
Bosi
wa benchi la ufundi la Yanga, Hans van Der Pluijm, amegoma kuzungumzia
nafasi ya beki na nahodha wa kikosi hicho, Nadir Haroub ‘Cannavaro’
ndani ya kikosi chake cha kwanza baada ya beki huyo kurejea akitokea
katika kipindi cha majeruhi.
Pluijm
raia wa Uholanzi alikuwa anamtumia Cannavaro katika kikosi cha kwanza
cha timu hiyo sambamba na Kelvin Yondani kabla ya kuumia ambapo nafasi
yake ikachukuliwa na Mtogo, Vincent Bossou.
Pluijm
alisema kuwa kwa sasa ni mapema kuanza kuzungumzia nafasi ya beki huyo
baada ya kurejea akitokea majeruhi ambapo anampa muda wa kujiweka sawa
kabla ya kumrejesha ndani ya kikosi hicho.
| PLUIJM NA MWAMBUSI |
“Kwa
sasa ni mapema kuanza kuzungumzia nafasi ya Cannavaro kwenye ‘first xi’
kwani kama unavyojua ndiyo kwanza amerejea kutoka nje alipokuwa
akisumbuliwa na majeraha ya kisigino.
“Nitakachokifanya
kwa sasa ni kumpa muda wa kujinoa zaidi na kujiweka sawa kwa ajili ya
kurejesha makali yake kwani kama unavyojua hajacheza kwa kipindi kirefu,
hivyo atafanya mazoezi hayo ya kujiweka sawa kabla ya baadaye
kumrejesha,” alisema Pluijm.

Hakuna maoni :