Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania bara mzunguko wa 17 unatarajiwa kuendelea kesho
Jumatano kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja mbalimbali, huku kila
timu ikisakapointi tatu muhimu kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Kesho
Jumatano, Simba SC watakua wenyeji wa maafande wa Mgambo Shooting
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, JKT Ruvu watawakaribisha
Mbeya City katika uwanja wa kumbukumu ya Karume Ilala, huku Mtibwa Sugar
wakicheza dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa Manungu – Turiani.
Jijini
Mbeya, Tanzania Prisons watakua wenyeji wa vinara wa ligi hiyo Young
Africans katika uwanja wa Sokoine, Wana kimanumanu African Sports
watacheza dhidi ya Mwadui FC uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku
wakata miwa wa Kagera Sugar wakiwakaribisha Majimaji FC katika uwanja wa
Kamabarage mjini Shinyanga.
Alhamisi
ligi hiyo itaendelea kwa kuchezwa mchezo mmoja tu, Wagosi wa Kaya
Coastal Union watawakaribisha Ndanda FC katika uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga.
Michezo
ya viporo ya Azam FC imepangiwa ratiba, mchezo dhidi ya Tanzania
Prisons utachezwa Februari 24 uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku
mchezo dhidi ya Stand United ukichezwa Machi 16 katika uwanja wa Azam
Complex.
IMETOLEWA NA TFF
Hakuna maoni :