SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / ENGLAND YATEUA KIKOSI KUWAVAA WAJERUMANI NA WADACHI KIRAFIKI.


ENGLAND-HODGSONMENEJA wa Timu ya Taifa ya England Roy Hodgson ameteua Kikosi cha Wachezaji 24 ili kuwavaa Mabingwa wa Dunia Germany na Netherlands kwenye Mechi za Kirafiki.

England watasafiri kwenda Berlin kucheza na Germany hapo Machi 26 na kisha kurejea kwao England Uwanjani Wembley Jijini London kucheza na Netherlands hapo Machi 29.

Miongoni mwa Wachezaji wapya walioitwa Kikosini ni Kiungo wa Miaka 26 wa Vinara wa Ligi Kuu England Leicester City, Danny Drinkwater, ambae ni mara ya kwanza kuitwa England.
Kepteni wa England, Wayne Rooney, hayumo Kikosini kwa vile bado anauguza Goti lake.

England - Idadi ya Wachezaji toka kila Klabu:
-Tottenham and Liverpool: 5
-Everton: 3
Man City, Leicester, Arsenal and Southampton: 2
Chelsea, Man United, Stoke: 1

Kikosi kamili cha England:
Makipa: Jack Butland (Stoke City), Fraser Forster (Southampton), Joe Hart (Manchester City).

Mabeki: Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Phil Jagielka (Everton), Danny Rose (Tottenham Hotspur), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Everton), Kyle Walker (Tottenham Hotspur).

Viungo: Dele Alli (Tottenham Hotspur), Ross Barkley (Everton), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Danny Drinkwater (Leicester City), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool), Raheem Sterling (Manchester City).

Mafowadi: Harry Kane (Tottenham Hotspur), Daniel Sturridge (Liverpool), Jamie Vardy (Leicester City), Theo Walcott (Arsenal), Danny Welbeck (Arsenal).

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply