Nahodha wa Simba, Hassan Isihaka ameomba radhi kwa kitendo alichomfanyia Kocha wake, Jackson Mayanja.
Isihaka
alimjibu kocha wake ‘mbovu’ wakati alipotaka kumpanga katika mechi
dhidi ya Singida United wakati alimtupa jukwaani katika mechi dhidi ya
Yanga.
Uongozi wa Simba, jana ulitangaza kumfungia kwa muda usiojulikana na kutokana na kitendo hicho cha utovu wa nidhamu.
Lakini leo, Isihaka ameuomba uongozi wa Simba kumsamahe.
“Kama
binadamu nimekosea, halikuwa lengo langu. Ninachoomba nisamehewe kama
mmoja wa wachezaji na vijana wa Simba,” alisema Isihaka.
Wadau wengi wa soka, wameonekana kufurahishwa na kitendo cha Isihaka kuamua kuomba radhi.
Hakuna maoni :