Beki wa pembeni wa Simba, Hassani Kessy, amewatoa hofu viongozi wa timu hiyo akiwaambia: “Leteni mkataba wenu.”
Kessy
ambaye amekuwa kwenye utata mkubwa katika mkataba wake na timu hiyo,
amesema yupo tayari kusaini mkataba na timu hiyo na wale wanaosema
amepewa mkataba akakataa kusaini ni waongo.
Beki
huyo hivi sasa ni mchezaji huru anayeruhusiwa kufanya mazungumzo na
klabu nyingine inayomhitaji kwa ajili ya kusaini mkataba kwa mujibu wa
kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Akizungumza,
Kessy alisema yeye hana tatizo na Simba na yupo tayari kuongeza mkataba
mwingine wa kuichezea timu hiyo kama watafikia makubaliano.
“Kiukweli
kabisa hakuna kiongozi yeyote wa Simba aliyenifuata na kunipa mkataba,
zaidi ni tetesi tu zinazozushwa ambazo siyo za kweli.
“Wao
hawatakiwi kuongea pembeni, wao wanachotakiwa kukifanya ni kunipa huo
mkataba kwa ajili ya kuusoma kwanza huku mazungumzo yakiendelea.
“Sasa
ninashangaa kusikia kuwa nimegomea mkataba Simba kitu ambacho siyo
sahihi, mimi ni mchezaji halali wa Simba ninayemaliza mkataba mwishoni
mwa msimu huu,” alisema Kessy.
Hakuna maoni :