SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / MAYANJA AELEZEA YANGA ITAKAVYOIMALIZA AL AHLY DAR ES SALAAM.


MAYANJA

Kiungo mchezeshaji wa zamani wa Al Masry ya Misri na Esprance ya Tunisia na kocha wa Simba kwa sasa, Mganda, Jackson Mayanja ‘Mia Mia’, amesema kitakuwa ni kichekesho cha mwaka kama Yanga itafungwa na Al Ahly ya sasa ambayo anaiona ‘vibonde’.

Licha ya uhasimu mkubwa kati ya timu yake na Yanga, lakini hilo si kigezo kwa Mayanja ambaye amesema Yanga ina bahati kubwa kwani Al Ahly ya sasa si ile anayoifahamu.

Imebadilika sana na ubora wao uko chini na kuongeza kuwa Yanga wana nafasi ya kuwondoa lakini kama kweli watajiandaa vema kutokana na asili ya soka la Kiarabu.

Yanga itaikaribisha Al Ahly Aprili 9, mwaka huu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, hata hivyo, takwimu zinaonyesha mara ya mwisho Waarabu hao walikubali kichapo kwenye Uwanja wa Taifa kabla ya kulipa kisasi huko kwao Cairo kisha kupenya kwa mikwaju ya penalti.

“Kitakuwa kichekesho kama Yanga itakubali kupoteza kwa Al Ahly hii ambayo nimeishuhudia mara kadhaa. Si ile Al Ahly ya Kiarabu niliyoijua, ile ilikuwa Al Ahly kweli, imejaza wachezaji mastaa ambao usingependa kukutana nao.


“Lakini nadhani machafuko ya kisiasa yamewaathiri sana, wanajipanga upya na bado hata ukiangalia mechi zao za hivi karibuni, utaona kabisa haina ubora ule wa asili ya soka la Kiarabu,” alisema Mganda huyo.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply