KESSY |
Suala
la beki wa Simba, Hassan Kessy limeingia kwenye sura nyingine kwa upande
wa benchi la ufundi la timu hiyo, baada ya kocha wa Wekundu hao,
Jackson Mayanja kuweka wazi msimamo wake kwamba yupo tayari kuona beki
huyo akitimka kikosini hapo.
Mayanja
ambaye ni raia wa Uganda aliyefanikiwa kurejesha hali ya ushindani
klabuni hapo kwa wapinzani wengine wa Ligi Kuu Bara, ameeleza hayo baada
ya kuwepo kwa suala la kusuasua kwa Kessy kuongeza mkataba wa
kuitumikia timu hiyo msimu ujao.
Mayanja
amesema kuwa, hakutakuwa na tatizo lolote iwapo beki huyo ataachana na
Klabu ya Simba kufuatia kuwa na wachezaji wengi watakaocheza nafasi
hiyo, hivyo hakutakuwa na pengo lake pindi atakapoondoka na kudai kuwa
timu hiyo ni kubwa kuliko mchezaji.
Aidha
alieleza kuwa, mpira wa sasa umebadilika tofauti na zamani ambapo
mchezaji anatakiwa kuwa huru kwa kuweka wazi kile anachojisikia kufanya.
“Kama
Kessy hataki kusaini mkataba mwingine haina haja ya kumlazimisha kwani
mpira wa sasa umebadilika tofauti na zamani, mchezaji wa kisasa anaweka
mambo yake hadharani kisha anaendelea kuitumikia timu yake hadi mkataba
wake utakapoisha kisha anaondoka.
“Wachezaji
kwa sasa wapo kimaslahi hivyo huwezi kumzuia na iwapo ataondoka kuna
wachezaji wengi ambao wataweza kushika nafasi yake kwani Simba ni klabu
kubwa kuliko mchezaji, mchezaji anaondoka na klabu inabaki.
“Mfano
mzuri tunaona wachezaji wa Ulaya mtu akitaka kuondoka anaweka wazi na
anaendelea kufanya kazi yake vizuri hadi atakapomaliza mkataba na
kuhamia timu nyingine,” alisema Mayanja.
“Mfano
Ronaldo aliondoka Man U na timu ikaendelea pia kuna wachezaji
mbalimbali Ulaya wameondoka katika timu zao na zimeendelea kufanya
vyema.
“Huwezi
kumlazimisha mchezaji abakie akiwa ameshaonyesha nia ya kuondoka aage
watu kwani inaweza kuwa tofauti huko mbele, hii ni ‘modern football’
kila kitu kinakaa wazi, naamini akiondoka yeye kuna wengine watakaoziba
nafasi yake.”
Hakuna maoni :