SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / TAMBWE AELEZA UGUMU WA APR LAKINI ASEMA WATAPAMBANA.


TAMBWE (WA PILI KULIA) AKIWA NDANI YA RWANDAIR NA KIKOSI KIZIMA CHA YANGA KWENDA KIGALI TAYARI KUIVAA APR.

Mshambuliaji nyota wa Yanga na kinara wa wapachika mabao Ligi Kuu Bara, Amissi Tambwe amesema haitakuwa kazi rahisi katika mechi yao dhidi ya APR, Jumamosi.

Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wameondoka leo kwenda jijini Kigali tayari kuwavaa wenyeji wao APR ya Rwanda.

Tambwe raia wa Burundi amesema, APR inapewa sapoti ya kutosha na Jeshi la Rwanda pamoja na Wanyarwanda lakini watapambana.

“Wanapewa sapoti kubwa sana, hii inafanya mechi iwe ngumu sana kwetu. Lakini kazi yetu ni kupambana kwa ajili ya timu yetu,” alisema Tambwe.

APR ambayo inajulikana kama “Watoto wa Kagame” kwa kuwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye ni mpenda michezo, ndiye shabiki namba moja wa timu hiyo.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply