Saa
chache baada ya Simba kuwasilisha barua yake kwa Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ikilalamikia viporo vya Yanga
na Azam FC, Bodi ya Ligi (TPLB) kwa kushirikiana na TFF zimetangaza
kufanya mabadiliko.
Mabadiliko
hayo yanaonyesha Yanga na Azam FC zitacheza viporo vyake haraka na
ndani ya siku 11, zitalazimika kucheza mechi tatu wakati Simba itacheza
mechi moja tu.
Yanga
na Azam FC zitalazimika kucheza mechi kuanzia Aprili 3, Aprili 6 na
Aprili 13 wakati huo Simba itacheza mechi moja tu ya Aprili 11. Maana
yake sasa timu hizo zitakuwa zimecheza mechi sawa kwa kuwa sasa zina
mechi 2 zaidi ya Simba.
Ndani ya kipindi hicho cha siku 11, Azam FC na Yanga watacheza mechi tatu na Simba itacheza mechi moja.
Aprili
3, Yanga itakuwa Dar es Salaam kuivaa Kagera Sugar na Azam FC itakuwa
ugenini CCM Kirumba jijini Mwanza kuivaa Toto African.
Aprili 6; Yanga itarejea dimbani Taifa kuivaa Mtibwa Sugar na Azam FC itakuwa Chamazi ikikaribisha Ndanda FC ya Mtwara.
Aprili
11, Simba nayo itashuka Uwanja wa Majimaji mjini Songea kuwa wageni wa
Majimaji, kwa maana hiyo, Yanga na Azam FC bado zitakuwa na mechi moja
kiporo tena.
Aprili
13, Yanga na Azam FC zitashuka “kubalance”, Yanga itacheza Mwadui FC
kwenye Uwanja wa Taifa na Azam FC itacheza dhidi ya Mtibwa Sugar ikiwa
ugenini Manungu, Turiani.
Hakuna maoni :