SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / YANGA YAREJEA KILELENI KWA KUZITIKISA NYAVU ZA AFRICAN SPORTS MARA 5 BILA MAJIBU.

TAMBWE
Ilikuwa kama utani, lakini sasa ni kweli kwamba Yanga imerejea kileleni baada ya kufikisha pointi 50.

Yanga imerejea kileleni mwa Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa African Sports ya Tanga kwa mabao 5-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ushindi huo ulikuwa muhimu kwa Yanga baada ya kuwa imeondolewa na Simba kileleni. Simba walifikisha pointi 48 baada ya kuitwanga Mbeya City kwa mabao 2-0.

Ubishi ukawa ni Simba itakaa kwa muda mfupi na wenye kilele ni Yanga. Kweli wamerejea baada  ya ushindi huo wa mabao 5-0.

Shukurani kubwa kwa Amissi Tambwe aliyefunga mabao mawili, Kelvin Yondani, Donald Ngoma na Anthony Simon Matheo ambao walikamilisha idadi hiyo ya “mkono” ya Yanga.
Mechi ilikuwa ya ushinda, Sports wakionekana wagumu katika dakika za mwanzo lakini kadiri muda unavyozidi kusonga mbele, wakazidi kupoteza mwelekeo na kutoa nafasi kwa Yanga “kufanya yao”.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply