SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / EL CLASICO: LEO KIVUMBI NOU CAMP, BARCA V REAL.

ELCLASICO-APR1LEO Uwanjani Nou Camp miamba ya Soka ya Spain, FC Barcelona na Real Madrid zinapambana kwenye Mechi ya La Liga ambayo Siku zote hubatizwa El Clasico.


FC Barcelona, ambao ndio Mabingwa Watatezi wa La Liga, wanatinga kwenye Mechi hii LALIGA-TOP-MAR29wakiwa Vinara wa Ligi hiyo wakiwa Pointi 10 mbele ya Timu ya 3 Real ambao wako Pointi 1 nyuma ya Timu ya Pili Atletico Madrid.

Hii ni El Clasico ya Pili Msimu huu baada ya ile ya Novemba 21 ambapo Real, wakiwa chini ya Meneja alietimuliwa Rafa Benitez, walinyukwa 4-0 na Barca Ueanjani Santiago Bernabeu.

Lakini Bosi wa sasa Real, Zinedine Zidane, hana presha yeyote ya ziada kuhusu El Clasico hii.

Zidane, akiingoza Real katika El Clasico yake ya kwanza, ameeleza: “Niko poa kabisa. Hii ni Gemu ya Soka na nitaifurahia. Sikosi usingizi. Tupo katika hali njema.”

Ukimuondoa Beki Raphael Varane ambae alikosa Mazoezi hapo Jana baada ya kuumia akiwa na Timu ya Taifa ya France, Zidane ana Kikosi kamili cha kuchagua Wachezaji wake 11 watakaoanza Mechi hii.

Nao Barca wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa hawajafungwa katika Mechi 39 mbio ilizoanzia Oktoba na Bosi wao, Luis Enrique, amesema nia yao ni kushinda Gemu hii.

Enrique ameeleza: “Tunacheza ili tubaki Vinara na tupige hatua kubwa kwenye Ligi. Haijalishi tuko Pointi ngapi mbele ya Real, sisi ni Timu Bora 2 Dunini!”
Kwenye El Clasico hii, kazi kubwa kwa Zidane ni kusaka njia ya kuwazuia Washambuliaji Mtu 3 za Barca, Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar, ambao wamebatizwa MSN, na ambao kati yao wamefunga Jumla ya Mabao 69 kwenye La Liga.

Lakini wenzao wa Real, Gareth Bale, Karim Benzema na Cristiano Ronaldo, wakijulikana kama BBC, wamefunga Bao 63 za La Liga huku Ronaldo ndie akitamba kuwa Mfungaji Bora wa Ligi hii akiwa na Mabao 28.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Barcelona (Mfumo 4-3-3):Bravo; Alves, Pique, Mascherano, Alba; Rakitic, Busquets, Iniesta; Messi, Suárez, Neymar
Real Madrid (Mfumo 4-3-3):Navas; Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo; Modric, Isco, Kroos; Benzema, Bale, Ronaldo

LA LIGA
Ratiba
**Saa za Bongo
Ijumaa Aprili 1
2130 Rayo Vallecano v Getafe CF
Jumamosi Aprili 2
1700 Atletico de Madrid v Real Betis
1915 Las Palmas v   Valencia C.F
2130 FC Barcelona v Real Madrid CF
2305 Celta de Vigo v Deportivo La Coruna
Jumapili Aprili 3
1200 Athletic de Bilbao v Granada CF
1600 Malaga CF v RCD Espanyol
1815 SD Eibar v Villarreal CF

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply