MAYANJA |
Kocha
Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja ameipigia hesabu kali mechi yake dhidi
ya Coastal Union itakayochezwa leo Jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
kwa kuhakikisha wanashinda mchezo huo huku akifurahia kurejea kwa
wachezaji wake nyota Hamisi Kiiza na Juuko Murshid waliokuwa katika
majukumu ya kitaifa.
Coastal
na Simba zitamenyana kwenye mchezo wa Kombe la FA katika hatua ya robo
fainali, wakiwa wanawania kuingia hatua ya nusu fainali huku timu za
Yanga, Azam na Mwadui zikiwa tayari zimeshaingia katika hatua hiyo.
Hata
hivyo, Kiiza ndiye mshambuliaji pekee wa Simba aliyefanikiwa kuzifunga
timu zote za Tanga msimu huu, hivyo kurejea kwake kunampa jeuri kocha
huyo kuiondoa Coastal katika hatua hiyo.
Mayanja
aliyewahi kuinoa timu hiyo amesema kikosi chake kipo fiti kuivaa
Coastal leo huku wachezaji wake nyota wakiwa tayari wamesharejea
kikosini.
“Nimejiandaa
vyema na kikosi changu kuelekea mechi yetu na Coastal, tunahitaji
kushinda mchezo huo ili kuweza kufanikiwa kuingia hatua inayofuata.
“Nashukuru
wachezaji wangu wapo vyema na Kiiza na Juuko tayari wamesharejea
kikosini na wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo huo,” alisema
Mayanja.
Hakuna maoni :