Timu
ya Mgambo ambayo juzi Jumatano ilipoteza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi
ya Yanga kwa kufungwa mabao 2-1, imekuwa na rekodi ya aina yake tangu
kwa mara ya kwanza ipande kucheza ligi kuu misimu minne iliyopita.
Mgambo
ilipanda ligi kuu msimu wa 2012/13 ambapo kwa misimu yote hiyo
haikuwahi kushuka daraja, lakini cha kushangaza ni kuwa imefanikiwa
kufunga mabao mawili tu ndani ya Uwanja wa Taifa, Dar kwa kipindi hicho
chote.
Awali,
timu hiyo ilicheza misimu mitatu mfululizo bila ya kuzifumania nyavu za
uwanja huo, mpaka walipokuja kuvunja mwiko huo msimu huu walipocheza na
Simba Februari 3, 2016 na kukubali kichapo cha mabao 5-1.
Straika
wao hatari, Fully Maganga, ndiye aliyefunga dhidi ya Simba na kuweka
rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kufunga bao kwenye Uwanja
wa Taifa, pia juzi Jumatano, Bolly Shaibu Ajally alifanikiwa kufunga
bao dhidi ya Yanga likiwa ni la pili kwa timu hiyo ndani ya misimu
minne.
Hakuna maoni :