KIUNGO
wa Simba, Mwinyi Kazimoto, leo anatarajiwa kufunga ndoa na mchumba wake
aliyefahamika kwa jina moja la Regina, hivyo hataichezea timu yake
dhidi ya Azam FC.
Simba
na Azam kesho Jumapili zinacheza mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja
wa Taifa, ambayo itatoa njia ya bingwa au timu itakayoshika nafasi ya
pili.
Kazimoto
anatarajiwa kufunga ndoa leo hii katika kanisa moja lililopo Kongowe
nje kidogo ya Dar es Salaam, hivyo hataweza kucheza mechi hiyo.
Kwa
upande wake Ibrahim Ajib, yeye ataikosa mechi hiyo kutokana na kuwa na
kadi tatu za njano alizopata katika mechi zilizopita za timu hiyo.
Kocha
wa Simba, Jackson Mayanja, alisema kukosekana kwa wachezaji hao ni pigo
kwake lakini amejipanga kuhakikisha anashinda mchezo huo.
Hakuna maoni :