Kocha
wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja amesema Yanga imepata jembe baada ya
kumsajili kiungo mshambuliaji wa Coastal Union, Juma Mahadh kutokana na
yeye kufahamu kiwango cha mchezaji huyo ambaye aliwahi kumfundisha kabla
ya kuhamia Simba.
Mahadh
ambaye ameonyesha kiwango kikubwa kwa msimu huu akiwa na Coastal Union
kiasi cha kuitwa timu ya taifa, Taifa Stars, amesajiliwa na Yanga kwa
mkataba wa miaka mitatu.
Mayanja
ambaye ameiongoza Simba kumaliza katika nafasi ya tatu katika msimamo
wa Ligi Kuu Bara amesema kuwa kutokana na kufahamu kipaji alichonacho
kiungo huyo ana uhakika mkubwa ataisaidia Yanga msimu ujao.
“Mimi
ndiye niliyemfanya Mahadh ajulikane kwani nilimkuta mtaani tu anacheza
lakini kwa uwezo aliokuwa nao ndiyo nikamvuta Coastal Union ambapo
ameonyesha uwezo wa hali ya juu mpaka sasa kusajiliwa na Yanga, jambo
ambalo kwangu najisikia furaha kuona linatokea.
“Naamini kwamba Yanga wamepata mchezaji sahihi, atawasaidia sana kwa msimu ujao kwani uwezo anao na anaweza kuwapa changamoto viungo wengine
Hakuna maoni :