HANS POPPE |
Ikiwa
ni siku chache baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kumtaka beki
Hassan Kessy kuondoa hofu kwa kuwa siku itafika atacheza, Mwenyekiti wa
Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema huenda beki huyo
akaendelea kubaki nje ya uwanja kwa msimu huu na mwingine.
Manji alisema hayo juzi huku akisisitiza, Kessy hawezi kutocheza milele.
Lakini
Hans Poppe amesema kinachomponza Kessy ni ujeuri wa viongozi wa Yanga
ambao wanajua wamekosea, lakini wanataka kuonyesha umwamba.
Akifanya
mahojiano na SALEHJEMBE jijini Dar es Salaam, Hans Poppe amesema Yanga
wanajua wamefanya makosa, lakini wanataka kuonyesha umwamba kama
walivyozoea.
“Waliwahi
kutufanyia hivi katika suala la Yondani, safari hii wamerudia na
kumsainisha Kessy wakati akiwa bado na mkataba na Simba.
“Kama
hiyo haitoshi, mkataba wameufikisha TFF, wameusajili na wakatuma Caf.
Sasa sisi tuna kila kitu na ushahidi mwingine wao wenyewe wameupeleka
TFF na Caf.
“Kilichotakiwa
ni kuandika barua, nilikutana na Chanji (kiongozi Yanga). Nikamweleza
andikeni barua mimi nitalisimamia hilo. Lakini hakufanya hivyo, wanataka
kuonyesha ujeuri.
“Kama
itaendelea hivi, ninaamini Kessy hatacheza. Na hapa wa kulaumiwa ni wao
maana Simba tupo hapa,” alisema Hans Poppe na alipoulizwa kama
wakiandika barua basi mara moja watamruhusu Kessy, akajibu.
“Wakiandika barua, basi sisi tuna jibu au majibu ya kuwapa. Sasa yatapatikana kutokana na barua yao.”
Hakuna maoni :