Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kila chama kifanye kampeni za kistaarabu ili kila mtu aende Ikulu pasipo kuvuruga amani.
Mbowe ameyasema hayo leo mbele ya waandishi wa habari wakati wa kuelezea masuala ya kampeni zinazoendelea kwa vyama vyote vya siasa, pia amesema kuwa kuna kauli za viongozi wa baadhi ya vyama ambazo haziridhishi katika kupigakwao kampeni.
Mbowe amasema kauli ya watu hao ni ya kichochezi na haiwezi kuvumilika lakini chama husika hakikuweza kufuta kauli hiyo.
Aidha amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekaa kimya kwa kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya vyama kuwa hawawezi kuachia watu wakatawale Ikulu.
Amesema kumekuwa na changamoto katika umoja wa katiba ya wananchi lakini hadi sasa mgogoro wa majimbo hauzidi 10 ambapo ni hatua nzuri kwa umoja huo nia yao ni kwenda Ikulu na sio kuwagwana majimbo kama sadaka.
Mbowe amesema tatizo la viongozi waandamizi NCCR-MAGEUZI, inatokana na kutaka majimbo wasimame licha kutambua mtu anapewa kugombea kutokana na sifa alizonazo pamoja na uwezo wa mtu kushinda katika uchaguzi mkuu.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)Freeman Mbowe leo makao makuu ya ngome ya UKAWA jijini Dar es Salaam leo
Hakuna maoni :