| UWANJA WA KAITABA... |
Uwanja
wa Kaitaba unakaribia kukamilika, timu ya Kagera Sugar imetoa onyo
mapema kwa timu za ligi kuu kuwa zisitegemee kuondoka na pointi hata
moja pindi Kagera itakaporejea kwenye uwanja huo.
Kaitaba
upo kwenye hatua za mwisho kukamilika ambapo mafundi wanamalizia
kumwaga mchanga maalumu kwenye nyasi, zoezi ambalo litachukua siku 10
kukamilika na kuwa tayari kwa kutumika.
| KAGERA |
Kocha
wa Kagera, Adolf Rishard ambaye timu yake imekuwa ikihamahama viwanja
tangu kuanza kwa matengenezo hayo, amenukuliwa akitoa majigambo hayo
juzi kisha akaongeza:
“Kucheza
Kambarage (Shinyanga) tunajihisi tupo ugenini japo ndipo tunapopatumia
kama uwanja wetu wa nyumbani, tukirudi Kaitaba kila atakayekuja ajue
kuwa hawezi kuondoka hata na pointi moja.”

Hakuna maoni :