Tiketi za Sh 7,000 katika pambano la Yanga dhidi ya Simba kesho, limezua zogo kubwa jijini Dar es Salaam.
Mashabiki
zaidi ya 100 walianza kulalamika wakida kuna mchezo mchafu kwamba
tiketi hizo zimeisha kwa kuwa kuna ulanguzi unafanyika makusudi.
Mashabiki
hao wameiambia SALEHJEMBE kwamba tiketi hizo zimeuzwa kwa saa moja
pekee, jambo ambalo wanaamini TFF itakuwa inafanya ujanja.
“Haiwezekani
tiketi ziishe ndani ya saa moja. Wanafanya makusudi baadaye watuuzie
kwa bei kubwa. Hatukubaliani na hili kwa kuwa sisi watu wa chini
tunaumia,” alisema Ibrahim Mohammed, mmoja wa mashabiki waliokuwa
wamekosa tiketi.
Kufikia saa 4 asubuhi, tiketi za Sh 7,000 zilikuwa zimeisha kila sehemu, hali iliyosababisha mzozo huo.

Hakuna maoni :