SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / YANGA WAWEKA REKODI, WALIPOTOKA PEMBA KABLA YA KWENDA KUIMALIZA SIMBA WALIKAA HOTELI YA AL AHLY, IVORY COAST.




Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski ni moja ya hoteli bora kabisa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Kawaida zimekuwa zikifikia timu za taifa za Ivory Coast, Misri na nyinginezo. Kwa upande wa timu Al Ahly ya Misri, mara kadhaa wamekuwa wakikataa kufikia hoteli walizopangiwa na Yanga au Simba na kwenda kukaa pale.

Katika hoteli hiyo yenye mazingira mwanana kila eneo, kawaida chumba ni kuanzia dola 248 (zaidi ya Sh 520,800) kwa siku. Safari hii, Yanga ndiyo walikuwa hapo.



Yanga walifikia kwenye hoteli hiyo na kuishi kwa siku moja, kabla ya kwenda na kuimaliza Simba kwa kuichapa kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa na kurejea kileleni.

Yanga walitua Kempinski wakiwa wanatokea Pemba ambako pia waliishi katika mazingira ya kitalii kabla ya kurejea Dar es Salaam tayari kwa mechi dhidi ya watani wao.







«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply