Kikosi
cha Azam FC kimeendeleza ushindi katika Ligi Kuu Bara baada ya kushinda
kwa maba 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja
wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Azam
ilianza Ligi Kuu Bara kwa kuichaa Prisons bao 2-1, ikaendeleza kipigo
cha 2-0 kwa Stand United kabla ya kuitandika Mwadui FC 1-0.
Sasa ina pointi 12 sawa na Yanga na Mtibwa Sugar ambazo hazijapoteza hata mechi moja katika nne zilizocheza.
Mabao
ya Azam FC katika mchezo huo yalifungwa na kiungo Mudathir Yahya katika
dakika ya 11 kabla ya Kipre Tchetche kumaliza kazi katika dakika ya 52.
Hata hivyo, Mbeya City walijitutumua na kupata bao katika dakika ya 55 kupitia kiungo wao Raphael Alpha.
Hata
hivyo, dakika za mwisho Mbeya City walionekana kukaa vizuri zaidi na
kuwahenyesha Azam FC ambao hata hivyo safu yao ya ulinzi ikiongozwa na
Serge Wawa ilionekana kusimama imara.
Hakuna maoni :