TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Tarehe 26-9-2015 jana Jumamosi kulifanyika
mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya timu yetu ya Simba Simba dhidi ya timu
ya Yanga.
Kwenye mchezo huo timu
yetu imepoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 2-0.
Tumeanza kuandika hivyo
hapo juu kwa makusudi kuonyesha sisi Simba tumeyakubali matokeo hayo ya dakika 90
za mchezo na tutumie nafasi hii kiungwana kabisa kuwapongeza watani wetu wa
jadi kwa ushindi huo walioupata.
Pili tumshukuru Mungu kwa
kutuwezesha kumaliza mchezo huo salama, na hapa Mungu ashukuriwe sana pamoja na
wapenzi wetu pia.
Sababu washabiki wetu
wameonyesha utulivu wa kiunamichezo kwa kutokufanya fujo yoyote licha ya
mwamuzi wa mchezo huo Israel Nkongo kuharibu mchezo kwa makusudi
Nkongo kwa dhamira ya
kusudi jana aliamua kuwatoa wachezaji wetu mchezoni kwa kuanza kugawa kadi kwa
wachezaji wetu pasi na sababu na kwa rafu zilezile kuacha wachezaji wa Yanga
kucheza bila kuwaonya.
Kilichoshangaza washabiki
wote waliokuwa uwanjani na walioangalia kwenye televisheni ni kumuacha mchezaji
wa Yanga Donald Ngoma kuendelea na mchezo ilhali alimpiga kichwa cha maksudi
mchezaji wetu Hassan kessy!
Mbali ya vitendo hvyo
wachezaji wetu wametulalamikia kutukanwa na mwamuzi wa mchezo huo Nkongo.
Tunaamini TFF watachunguza
malalamiko yetu na kuchukua hatua stahiki kwa mwamuzi huyo ambaye kila mtu
aliyeuona mchezo huo anakiri kuwa alishindwa kuumudu.
Mwisho na kwa umuhimu wa
kipekee klabu ya Simba inaendelea kuwashukuru washabiki kwa utulivu wao licha
ya vitendo vya mwamuzi huyo ambavyo vingeweza kabisa kuharibu amani iliyokuwepo
uwanjani jana.
Hakuna maoni :