SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / BRAZIL WAMTOA FIRMINO KIKOSINI, WAMWITA MKONGWE WA MIAKA 35 OLIVEIRA!



BRAZIL-RICARDO-OLIVEIRAFOWADI wa zamani wa Valencia, Real Betis, AC Milan na Zaragoza ambae sasa ndie anaongoza katika Ufungaji Bora huko Brazil ameitwa kumbadili Straika wa Liverpool Roberto Firmino kwenye Kikosi cha Brazil kitakachocheza Mechi za Kundi lao la kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Straika wa Santos Ricardo Oliveira, mwenye Miaka 35, ameitwa kuzikabili Chile na Venezuela kwenye Mechi za Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini zinazoanza Oktoba.

Firmino ameondolewa Kikosini baada ya kuumia Jumatano Usiku akiichezea Klabu yake Liverpool ilipocheza na Carlisle kwenye Mechi ya Raundi ya 3 ya Capital One Cup na kushinda kwa Mikwaju ya Penati 3-2 baada ya Sare ya 1-1.
Msimu huu, Oliveira ameifungia Santos Bao 17 katika Ligi kubwa ya Brazil lakini hajaitwa kuichezea Brazil tangu Mwaka 2007.

Kocha wa Brazil Dunga alitangaza Kikosi chake cha Brazil mapema Mwezi huu ambacho Oktoba kitaanza safari ya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2018 huko Russia.

Brazil, ambao ni washika Rekodi kwa kutwaa Ubingwa wa Dunia mara 5, wanacheza Mechi za Mchujo za Kanda ya Marekani ya Kusini na Mechi yao ya kwanza ni huko Santiago Nchini Chile hapo Oktoba 8 dhidi ya Wenyeji Chile ambao ndio Mabingwa wa Copa America.
Tarehe 13 Oktoba, Brazil watakuwa kwao hukoFortaleza kucheza na Venezuela katika Mchujo huo.

Kwenye Mechi hizo mbili za Brazil, Neymar, Kepteni wa Brazil, ameachwa kwa vile yupo Kifungoni na kutoruhusiwa kucheza Mechi hizo kufuatia kufungiwa kwenye Fainali za Copa America huko Chile Mwezi Julai.

BRAZIL-KIKOSI KAMILI KILICHOTANGAZWA SEPTEMBA 18:
MAKIPA: Jefferson (Botafogo), Marcelo Grohe (Gremio), Alisson (Internacional)
MABEKI: David Luiz (PSG), Miranda (Inter Milan), Marquinhos (PSG), Gil (Corinthians), Fabinho (Monaco), Rafinha (Bayern Munich), Filipe Luis (Atletico Madrid), Marcelo (Real Madrid)

VIUNGO: Luiz Gustavo (Wolfsburg), Fernandinho (Manchester City), Elias (Corinthians), Renato Augusto (Corinthians), Lucas Lima (Santos), Philippe Coutinho (Liverpool), Oscar (Chelsea), Willian (Chelsea), Douglas Costa (Bayern Munich)
MAFOWADI: Hulk (Zenit Saint-Petersburg), Roberto Firmino (Liverpool), Lucas (PSG)

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply