SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / DABI YA KARIAKOO: KUELEKEA MTANANGE JUMAMOSI SIMBA v MABINGWA YANGA!



VPL-SIMBA-YANGAJumamosi, Barabara zote za Jiji la Dar es Salaam zitaelekea Uwanja wa Taifa kushuhudia Klabu kongwe Nchini Tanzania, Simba na Yanga, zenye Makao Makuu yao Eneo la Kariakoo Jijini humo, zikipambana katika pambano la Ligi VPL-STAND-SEP26Kuu Vodacom, VPL.
Msimu huu, Timu zote zikiwa chini ya Makocha wa Kigeni zimeanza kwa moto mkali na zote zimeshinda Mechi zao 3 za mwanzo za VPL.
Yanga, chini ya Mholanzi Hans van Pluijm akisaidiwa na Kocha wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa, ndio Mabingwa Watetezi wa VPL na ndio wanaoongoza Ligi hii wakiwa Pointi sawa na Simba lakini wao wana ubora wa Magoli.
Simba wao wako chini ya Kocha Mwingereza Dylan Kerr akisaidiwa na Seleman Matola na safari hii wameanza kwa ukali unaoongozwa na Mshambuliaji wao kutoka Uganda Hamisi Kiiza ambae sasa ndio anaongoza ufungaji kwenye VPL akiwa na Bao 5.
Lakini tofauti na Simba, Mabao mengi ya Yanga kwenye VPL yametokana na Washambuliaji wao wawili wa Kigeni, Donald Ngoma na Amisi Tambwe, ambao wote wamepiga Bao 3 kila mmoja.

VIINGILIO:
-VIP A: Sh. 30,000/=
-VIP B & C: Sh 20,000/=
-VITI RANGI YA BLU, KIJANI & ORANGE: Sh 7,000/=
MAUZO TIKETI:
-Kuanza kuuzwa-Leo Ijumaa Saa 2 Asubuhi
-VITUO:
-Karume – Ofisi za TFF
-Buguruni – Oilcom
-Dar Live – Mbagala
-Uwanja wa Taifa
-Luther House – Posta
-Ferry – Kivukoni
-Mnazi Mmoja
-Ubungo – Oilcom
-Makumbusho – Standi ya Mabasi ya Daladala.


Timu hizi kwa sasa zimejichimbia Visiwani ambako Yanga wako Pemba na Simba wako huko Zanzibar.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
SIMBA: Peter Manyika,Mohammed Hussein‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Hassan Kessy, Said Ndemla, Justice Majibva, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Hamisi Kiiza, Peter Mwalyanzi
YANGA: Ali Mustapha ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Haji Mwinyi, Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaeseke, Simon Msuva, Donald Ngoma, Amisi Tambwe
MAREFA:
-Refa Mkuu: Israel Nkongo (Dsm)
-Marefa Wasaidizi: Josephat Bulali (Tanga), Ferdinand Chacha (Mwanza)
-Mwamuzi wa Akiba: Soud Lila (Dsm)
-Kamisaa: Charles Mchau (Kilimanjaro)
LIGI KUU VODACOM
RATIBA
Jumamosi Septemba 26
Simba v Yanga
Coastal Union v Mwadui
Tanzania Prisons v Mgambo Shooting
JKT Ruvu v Stand United (Uwanja wa Karume, Dar es salaam)
Mtibwa Sugar v Majimjaji
Kagera Sugar v Toto Africans (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora)
Jumapili Septemba 27
Azam FC v Mbeya City
African Sports v Ndanda FC


«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply