Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma amesema mechi dhidi ya Simba, itakuwa kama mechi nyingine na ana uhakikaa atafunga.
Ngoma
raia wa Zimbabwe, amefikisha mabao matatu katika mechi zake tatu za
Ligi Kuu Bara. Mechi ya nne ni dhidi ya Simba, wikiendi ijayo.
"Nimeanza
kuona ugumu wa ligi, lakini ninaona pia napata uzoefu na kujua cha
kufanya. Simba ni watani wa Yanga lakini ni timu kama nyingine.
"Kufunga
hakuwezi kuwa asilimia mia, lakini ninaamini uwezo wangu, ninawaamini
wenzangu na ninaiamini timu kwa ujumla na ushirikiano wetu.
"Litakalotokea kama ni kufunga au kutoa pasi, lakini kikubwa Yanga ishinde ili twende na mwendo huu," alisema Ngoma.
Hakuna maoni :