KOCHA wa Manchester United, Louis van Gaal amesema kwamba beki wake Luke Shaw atakuwa nje mwa muda usiopungua miezi sita baada ya kuumia jana katiia mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya wenyeji PSV nchini Uholanzi.
Katika
mchezo huo ambao United ililala 2-1, Shaw alimwaga machozi wakati
wanatolewa nje kutokana na uchungu wa maumivu makali kutokana na
kuvunjika mguu wake wa kulia.
Dunia
ya soka iliungana usiku wa jana baada ya beki wa PSV Eindhoven, Hector
Moreno kumvunja mara mbili mchezaji wa kimataifa wa England mwenye umri
wa miaka 20 mguu wa kulia.
Shaw
aliwekewa hewa ya ziada na kupatiwa huduma ya kwanza uwanjani mjini
Eindhoven kabla ya kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi. Atarejeshwa
Manchester leo na Alhamisi anatarajiwa kufanyiwa upasuaji.
Beki
wa Manchester United, Luke Shaw akiugulia maumivu baada ya kuumia mguu
jana katika mchezo dhidi ya wenyeji PSV Ligi ya Mabingwa Ulaya PICHA ZAIDI GONGA HAPA


Hakuna maoni :