Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo cha Uandishi wa Habari na
Utangazaji Arusha [AJTC] Bw. Joseph Mayagila amewataka wanafunzi wa chuo hicho
kutumia fursa za biashara pindi wawapo chuoni hapo ili waweze kupambana na changamoto
za maisha watakapomaliza masomo yao.
Mkurugezi huyo amesisitiza hilo leo wakati akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwenye ukumbi
wa chuo hicho nakusema kuwa wanafunzi wasisome ili waajiriwe tu kwani wapo
wanafunzi wengi ambao wamemaliza masomo
yao lakini hawana ajira na wanaendeleza maisha yao vizuri kupita ujasiramali.
Bw. Mayagila amesema
watu wengi wenye mafanikio makubwa duniani
ni wajasiriamali wakubwa na wadogo hivyo aoni ajabu kwa mwanafunzi yeyote
atakaeshika mafunzo anayopewa bure chuoni hapo kuja kuwa mjasiriamali mkubwa
pia.
‘’Mimi nimefundisha semina mbalimbali za ujasiriamali na
huwa napata majibu mazuri kwa wale ninaowafundisha kikubwa katika ujasiria mali
ni kujua jinsi ya kutumia one hour habit per day [kujiwekea muda wa lisaa
limoja kila siku kusoma kwa kile unachokilenga] hapo ndipo utaweza kufanikiwa.’’
Alisema Mayagila.
Mkurugenzi huyo amewataka wanafunzi waondokane na dhana ya
kununua tu pasipo kuuza kwani kufanya hivyo ni kupalilia umasikini hata kama
mtu ni mwajiriwa katika sekta kubwa akitaka kuendelea ni lazima awe muuzaji wa
huduma pamoja na bidhaa.
‘’Tanzania ina rasilimali nyingi kuliko Kenya lakini nchi ya
Kenya wametupita kiuchumi kutokana na kukua kwa soko lao la mauzo kwa nchi za Afrika Mashari na Dunia kwa ujumla na hii inatokana
na Kenya kutambua ili uchumi wao kukua ni lazima kuwepo kwa soko la kuuza.’’ Aliseme
Joseph.
Semina ya ujasirimali chuoni hapo hufanyika kila mwaka na
kipindi hiki itafanyika kwa siku mbili
na Wakufunzi wa chuo hicho pamoja na waliofanikiwa kupitia ujasiriamali toka nje ya chuo hicho kuwafundisha
wanafunzi ni kwa jinsi gani wanaweza kuwa na mafanikio makubwa kupitia ujasiriamali,
na wenge wao waliomaliza masomo chuoni hapo wanafanya biashara zao kutokana na mafunzo
hayo.
Hakuna maoni :