SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / WANAFUNZI WASHAURIWA KUONDOKANA NA WAZO LA KUAJIRIWA TU WAMALIZAPO MASOMO YA VYUONI NA BADALA YAKE WAJIHUSISHE NA UJASIRIAMALILI.




            Bwana Josephu Mayagila akiwa katika Semina ya Ujasiriamali.

Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha [AJTC] Bw. Joseph Mayagila amewataka wanafunzi wa chuo hicho kutumia fursa za biashara pindi wawapo chuoni hapo ili waweze kupambana na changamoto za maisha watakapomaliza masomo yao.


Mkurugezi huyo amesisitiza hilo leo wakati  akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwenye ukumbi wa chuo hicho nakusema kuwa wanafunzi wasisome ili waajiriwe tu kwani wapo wanafunzi  wengi ambao wamemaliza masomo yao lakini hawana ajira na wanaendeleza maisha yao vizuri kupita ujasiramali.


Bw. Mayagila  amesema watu wengi wenye mafanikio  makubwa duniani ni wajasiriamali wakubwa na wadogo hivyo aoni ajabu kwa mwanafunzi yeyote atakaeshika mafunzo anayopewa bure chuoni hapo kuja kuwa mjasiriamali mkubwa pia.


‘’Mimi nimefundisha semina mbalimbali za ujasiriamali na huwa napata majibu mazuri kwa wale ninaowafundisha kikubwa katika ujasiria mali ni kujua jinsi ya kutumia one hour habit per day [kujiwekea muda wa lisaa limoja kila siku kusoma kwa kile unachokilenga] hapo ndipo utaweza kufanikiwa.’’ Alisema Mayagila.


Mkurugenzi huyo amewataka wanafunzi waondokane na dhana ya kununua tu pasipo kuuza kwani kufanya hivyo ni kupalilia umasikini hata kama mtu ni mwajiriwa katika sekta kubwa akitaka kuendelea ni lazima awe muuzaji wa huduma pamoja na bidhaa.


‘’Tanzania ina rasilimali nyingi kuliko Kenya lakini nchi ya Kenya wametupita kiuchumi kutokana na kukua kwa soko lao la mauzo kwa nchi za  Afrika Mashari na Dunia kwa ujumla na hii inatokana na Kenya kutambua ili uchumi wao kukua ni lazima kuwepo kwa soko la kuuza.’’ Aliseme Joseph.


Semina ya ujasirimali chuoni hapo hufanyika kila mwaka na kipindi hiki itafanyika kwa siku mbili  na Wakufunzi wa chuo hicho pamoja na waliofanikiwa  kupitia  ujasiriamali toka nje ya chuo hicho kuwafundisha wanafunzi ni kwa jinsi gani wanaweza kuwa na mafanikio makubwa kupitia ujasiriamali, na wenge wao waliomaliza masomo chuoni hapo  wanafanya biashara zao kutokana na mafunzo hayo.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply