FA,
Chama cha Soka England, kimetakiwa kichunguze kwa nini Straika wa
Chelsea Diego Costa ameepuka kupewa Kadi Nyekundu katika Mechi yao ya
Ligi Kuu England iliyochezwa Leo Stamford Bridge na Chelsea kuifunga Mtu
9 Arsenal Bao 2-0.Katika Mechi hiyo, Sentahafu wa Arsenal Gabriel alitolewa kwa Kadi Nyekundu baada ya kumtia Teke Costa na baadae Kipindi cha Pili Arsenal walibaki Mtu 9 baada ya Kiungo wao Santi Cazorla kupewa Kadi za Njano 2 na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Wenger amesema: “Huyu Costa atafanya hivi hivi Wiki ijayo na Wiki inayofuata na Siku zote hukwepa Kadi!”
Wenger alieleza: “Siku zote Costa anafanya anachotaka na anabaki Uwanjani lakini wengine wote wakijibu uchokozi wake wanatolewa nje. Alimpiga Koscielny usoni na hakufanywa kitu. Costa ametumia udhaifu wa Refa Mike Dean.”
Lakini Jose Mourinho amejibu tuhuma hizo za Wenger kwa kudai Wenger Siku zote hulalamika tu: “Nimechezea na Wenger mara 15 na mara pekee hakulalamika ni tulipofungwa kwenye Ngao ya Jamii!

Hakuna maoni :