SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / Askofu Gwajima amuonya Abdalah Bulembo na CCM waache kumchokoza mara moja.....Wakiendelea Atajibu Mapigo na Nchi Itatikisika



Askofu  mkuu  wa  Kanisa  la Ufufuo  na  Uzima, Rev.  Josephat   Gwajima ametoa  Onyo  kali  kwa  mwenyekiti  wa  Jumuiya  ya  Wazazi  ya  CCM (taifa),  bwana Abdallah  Bulembo  kwa  kulitaja  jina  lake  katika  mkutano  wa  kampeni  za CCM  huko  Singida.

Onyo  hilo  limetolewa  jana  na  Askofu  Gwajima  mbele  ya  waumini  wake  huku  akimtahadharisha  Bulembo  kuwa  iwapo  ataendelea, basi  na  yeye  ataibuka kutoka   mafichoni  ili kujibu  mashambulizi.

"Nakuonya  Bulembo, uache  kunitaja  kwenye  mikutano  yenu  ya kampeni.Ukiendelea  kunitaja,  nitapanda  helkopta  nikufuate  huko huko  ili  nijibu  mapigo. Sitakujibu  peke  yako, ntawajibu  na  waliokutuma.

"Nawatuma  watu  wa  CCM  mliopo  kanisani  kwangu  mmwambie  Bulembo  aniache. Nikimjibu  atasikitika.
"Nikiwajibu, utatoka  moshi  na  hawatafungua  macho. Ntawajibu  wote  na  waliomtuma  hadi  nchi  itatikisika."-Gwajima

Akiwa  mkoani  Singida  kwenye  mikutano ya  kampeni  za  mgombea  urais  wa  CCM, Dr. John Pombe  Magufuli, Bulembo  anadaiwa  kumtuhumu  Gwajima  kwa kuandaa machafuko ili kuharibu  amani  ya  nchi.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply