SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / CANNAVARO AMJIBU BOCCO; “KUIFUNGA YANGA HII NDOTO, SISI NDIYO TUTAWAFUNGA NYINYI”




NAHODHA wa Yanga SC, Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ amejibu tambo za Nahodha wa Azam FC, John Raphael Bocco ‘Adebayor’.

Bocco alikaririwa na blog hii
jana akisema kwamba wataifunga Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Lakini Cannavaro amemjibu; “Hizo ni ndito za mchana, sisi ndiyo tutawafunga wao,”amesema Cannavaro ambaye pia ni Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars akizungumza na blog hii jana
Nahodha wa Yanga na Taifa Stars, Nadir Haroub 'Cannavaro' kulia amesema wataifunga Azam FC Jumamosi

“Sisi kwa kweli timu yetu imezidi kuimarika msimu huu na ninaamini Azam FC tutawafunga Jumamosi, wakibahatika sana watapata sare, na hiyo sare waitolee jasho haswa,”amesema.
Juzi Bocco alisema; “Tunawajua Yanga, ni timu nzuri kweli. Lakini sisi tunajua namna ya kuwafunga. Na tutawafunga tu,”.
Mechi mbili za awali msimu huu kuzikutanisha Yanga na Azam FC kila timu ilishinda moja, tena kwa mikwaju ya penalti.  

Azam FC ilianza kuifunga Yanga SC kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati, Kombe la Kagame Julai mjini Dar es Salaam.
Na Yanga SC ikalipa kisasi kwa ushindi wa penalti 8-7 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 katika mchezo wa Ngao ya Jamii Uwanja wa Taifa Agosti mwaka huu.

Jumamosi zikikutana kwa mara ya tatu, utakuwa mchezo wa kuwania usukani wa Ligi Kuu na pia kumaliza ubishi wa nani zaidi baina yao.

Kwa ujumla Ligi Kuu inandelea Jumakosi kwa mechi sita kupigwa kwenye viwanja tofauti na mbali na Yanga SC kumenyana na Azam FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam- Majimaji FC wataikaribisha African Sports Uwanja wa Majimaji, Songea na Mbeya City watakuwa wenyeji wa Simba SC Uwanja wa Sokoine, Mbeya

Ndanda FC wataikaribisha Toto Africans Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, Stand United wataikaribisha Prisons Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na Coastal Union watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, wakati Jumapili Mgambo Shooting wataikaribisha Kagera Sugar Mkwakwani na Mwadui FC watakuwa wenyeji wa JKT Ruvu Uwanja wa Mwadui Complex.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply