Kamati
ya kuisaidia Taifa Stars imetangaza kauli mbiu ya ushindi inayosema
“NCHI YETU, TIMU YETU, TAIFA LETU, USHINDI WETU” itakayoanza kutumika
kuanzia leo hii.
Kamati hiyo chini ya uenyekiti wa Farouk Baghoza imemteua Bi Teddy Mapunda kuwa msemaji mkuu wa kamati hiyo.
Timu
inatarajia kuweka kambi Nje ya Nchi kwa takribani siku 12 ili kujiandaa
na mechi dhidi ya Algeria Novemba 14 Dar es salaam, na Novemba 17
nchini Algeria.
Aidha,
Mwenyekiti alitumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania wote warudishe
imani kwa timu yao, wajitokeze kwa wingi kwenye mechi ijayo tarehe 14
November dhidi ya Algeria hapa nyumbani.
Hakuna maoni :