SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / Kauli ya Mchungaji Mtikila Siku Moja Kabla ya Kifo Chake 'Msipige kura Oktoba Kumchagua Rais ili Nigombee Urais'


MWENYEKITI wa chama cha DP Mch. Christoper Mtikila siku moja kabla ya kifo chake aliwataka wakazi wa mkoa wa Njombe kuto chagua rais baada ya kuingia katika chumba cha Uchaguzi Octaba 25 mwaka huu kwa kuwa yeye wagombea uraisi wote walio simamishwa na vyama vingine hapa nchini anaona wanadosari.

Marehemu Mtikila Aliyasema hayo katika viwanja vya National Housing vya mjini Njombe wakati akizungumza na wakazi wa Njombe katika mkutano wa Kampeni za kuwanadi wagombea wa Chama chake cha Dp kwa ngazi za Ubunge na Udiwani.

Mtikila alisema kuwa wagombea wote walio simamishwa kumpokea Rais Jakaya Kimwete wote anaona hawafai kuipokea Tanzania na kuwa hawana ukombozi wa kweli kwa watanzania. "Wote walio simamishwa kutaka kutuongoza hata weza kuikomoa nchi yetu mniombee nifanikiwe rufaa yangu na mishine msipidge kura ya Rais pigeni kura za wabunge ambao mnawaamini ili uchaguzi urudiwe na mimi nikichukua fomu ninaimani nitashinda," alisema Marehemu Mtikila.

Aliwataka wakazi wa Njombe kuto pigia kura Rais Yoyote siku ya uchaguzi kitu kitakacho sababisha uchaguzi kuahirishwa na mchakato kuanza upya na yeye kuingia katika kinyanganyilo cha kuusaka Urais na akishinda ataleta ukombozi wa kweli kwa watanganyika.

Alisema kazi yoyote mtu anayomba anaenda kuchunguwa kama ni mzima lakini fomu za mwaka huu hakuna aliyeenda kuchunguzwa nashangaa, miaka ya nyuma wakati anenda kuchukua formu ya Uraisi niliambiwa niende Muhimbili kuchunguzwa afya yangu.

Alisema kuwa watu wanaenda kuchunguzwa kwa kuwa ugonjwa wowote unaleta itirafu katika kichwa na kushindwa kufanya kazi vizuri.

"Kazi yoyote unavyoomba unaenda Hospitalini Kuchunguzwa kwa kuwa mtu ukiwa na ugomjwa wowote Mwilini mwako unasababisha madhara katika kichwa kwa sababu hata ukiganyaga kipisi cha sigala kama mvutaji alikitupa vibaya akili inapiga simu haraka katika mguu wako na kukutaka uondoe hiyo mtu akiwa anaumwa hataweza kuwa vizuri kutokana na madhara ya ugonjwa,"

Alisema kuwa mtu akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wowote Nyaya hugusana na hivyo mtu kama hakuenda kupima na kama anaumwa anaogopwa kuajiliwa kwa kuwa atasababisha hasara kwa kuwa nyaya zitakuwa zinagusana. Alisema kuwa watu wanao jaza watu wanawajaza kwa kuwanunulia viroba na kuwa haita wezekana kumpata raisi mweye ukombozi wa taifa hili kama kutakuwa na watu anawanunulia viroba ili waje kwenye mikutano yake.

Alisema kuwa yeye hajajaza watu katika mikutano yake kwa kuwa hawanunulii viroba, lakini alijipo moyo kwa kusema kuwa watanzania waliopo katika mkutano wake ndio watakao sambaza taarifa za ukombozi kwa wale ambao hawapo katika mkutano huo.

Marehemu Mtikija Jana Kabla ya kifo chake leo Alfajiri alimnadi mgombea wa Ubunge kupitia chama chake Cha DP jimbo la Njombe Kusini William Myegeta na kuwataka wananchi kumchagua mhombea huyo kwa lengo la kiigomboa Njombe na Tanzania kwa ujumla. Alisema kuwa Chama hicho kimesimamisha wagombea katika majimbo mengi na sio Njombe Pekee na kuahidi kuwa atazunguka nchi nzima kuwanadi wagombea hao.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply