SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / MOURINHO 'KUTI KAVU' - ANG'AKA: "MKITAKA NIONDOKE NITIMUENI, SITABWAGA MANYANGA!"





MOURINHO-ALIZWA-SAINTSJose Mourinho amedai hataachia ngazi kwa hiari yake kama Meneja wa Chelsea labda afukuzwe kazi.
Jana Chelsea, ikiwa Nyumbani kwao Stamford Bridge, ilitandikwa 3-1 na Southampton katika Mechi ya Ligi Kuu England ambayo wao ndio Mabingwa Watetezi.
Kipigo hicho ni cha 4 kwa Chelsea katika Ligi katika Mechi 8 ambazo wameshinda 2 tu na Sare 2 na sasa wako Nafasi ya 16 wakiwa Pointi 10 nyuma ya Vinara Man City.
Akiongea mara baada ya kipigo cha Jana, Mourinho alisema: "Nataka niweke wazi. Kwanza sikimbii. Pili, Kama Klabu inataka kunifukuza wanifukuze tu ila mimi sitakimbia wajibu wangu na Timu yangu!"
Mourinho aliongeza: "Kuwa Bingwa kwa sasa ni ngumu kwa sababu tuko nyuma mno. Lakini nina hakika tutamaliza tukiwa ndani ya 4 bora. Msimu ukiwa mbovu ukimaliza kwenye 4 bora ni sawa."
Mourinho alinena: "Hiki ni kipindi kigumu na muhimu kwenye historia ya Klabu hii. Unajua kwa nini? Kwa sababu wakinifukuza mimi watakuwa wamemfukuza Meneja bora Klabu hii imewahi kumpata!"
Mourinho ameitumikia Chelsea katika Vipindi viwili tofauti na cha kwanza ni kile cha 2004 hadi 2007 na kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 2.
Kisha Mourinho akarudi tena Chelsea 2013 na Msimu uliopita kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England.

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply