SIASA

SIASA

MAONI

MAONI

BURUDANI

MICHEZO

/ / KLABU BINGWA AFRIKA-FAINALI: SAMATTA, ULIMWENGU JUMAMOSI VITANI NA TP MAZEMBE HUKO ALGERIA!


MAZEMBEKLABU ya Algeria USM Alger inasaka Taji lake la kwanza la Ubingwa wa Afrika hapo Jumamosi huko kwao Algiers ambako watakuwa Wenyeji wa TP Mazembe ya Congo DR katika Mechi ya Kwanza ya Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI.

Lakini USM Alger ina kibarua kigumu kwani TP Mazembe, ikiwa na Mastraika hatari kutoka Tanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, ni Timu ngumu yenye uzoefu ambayo imeshatwaa Mataji Manne ya Afrika na katika Mashindano 6 yaliyopita ya CAF CHAMPIONZ LIGI imeshatinga Nusu Fainali mara 4.

TP Mazembe ni Klabu yenye Makao Makuu huko Jimbo la Katanga Nchini Congo DR ambalo ni Tajiri kwa Madini ya Shaba na inamilikiwa na Gavana wa Jimbo hilo Moise Katumbi.

Hivi sasa TP Mazembe ipo chini ya Kocha aliewahi kuichezea St Etienne ya France, Patrice Carteron ambae amekuwa akikisuka Kikosi chake kwa Wiki Moja sasa Kambini huko Marrakesh, Morocco.

USM Alger na TP Mazembe zimetinga Fainali hii kwa kuzibwaga Klabu za Sudan kwenye Nusu Fainali.

Marudiano ya Fainali hii ni Novemba 8 huko Lubumbashi, Congo DR.
Mshindi wa Fainali hizi ataiwakilisha Afrika kwenye Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani huko Japan Mwezi Desemba.

CAF CHAMPIONZ LIGI
FAINALI
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 31
2230 Union Sportive Medina d’Alger [Algeria] v TP Mazembe [Congo, DR]
Marudiano
Jumapili Novemba 8
1630 TP Mazembe v Union Sportive Medina d’Alger

«
Next

Chapisho Jipya

»
Previous

Taarifa za zamani

About Unknown

Asante kwa kutembelea SELASINI HABARI,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA SELASINIHABARI.BLOGSPOT.COM.

Hakuna maoni :

Leave a Reply